skip to main |
skip to sidebar
Deni la Taifa limepanda kutoka trilioni 16.98 cha mwaka wa fedha 2011/2012 hadi kufikia trilioni 21.2 kiwango ambacho kikigawanywa kwa kila Mtanzania kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh,
ameweka hadharani deni hilo wakati akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa
fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni.
Utouh amesema ongezeko hilo limesababishwa na mikopo kutoka kwenye
mabenki na nchi wafadhili kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya
maendeleo.
Utouh amesema deni la nje limefikia Sh. trilioni 15 hadi Juni 30, 2013
ambalo ni ongezeko la Sh. trilioni 3.0 kutoka Sh. trilioni 12.43 kwa
mwaka 2011/12, wakati lile la ndani limefikia Sh. trilioni 5.78 ikiwa ni
ongezeko la Sh. trilioni 1.23 kutoka Sh. trilioni 4.55 kwa mwaka
2011/12.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe,
amepongeza ukaguzi huo kubaini mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kunusuru
fedha za walipakodi ambapo amesema kuwa ripoti hiyo itaanza kufanyiwa
kazi kuanzia sasa hadi Novemba ili kutoa maelekezo kwa hatua mbalimbali
ambazo serikali itapaswa kuzichukua.Na Dodoma Fm
No comments:
Post a Comment