Pages

Wednesday, May 21, 2014

DIAMOND AINGIA TENA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA TUZO NYINGINE

Tuzo za watu
Na.Mwandishi wetu, Dar es Salaam,
Tarehe 29 April, Bongo5 Media Group ilizindua rasmi tuzo za watu Tanzania kwa mwaka 2014. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kuanza rasmi kwa mchakato wa kupendekeza majina yatakayoingia kwenye tuzo za mwaka huu. Wananchi walishiriki kupiga kura kupitia njia ya mtandao kwenye tovuti ya TUZO ZETU, na kwa njia ya ujumbe mfupi wa  simu za mkononi.
Awamu ya kwanza ya upigaji kura iliyodumu kwa wiki mbili na siku kadhaa imekua ikikusanya majina matano kwenye kila kipengele kama ifuatavyo;

MAJINA YA TUZO ZA WATU YALIYOPATIKANA KUTOKANA NA MAPENDEKEZO YA WANANCHI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
1. Vanessa Mdee – Choice FM
2. Millard Ayo – Clouds FM
3. Hamis Mandi aka B12 – Clouds FM
4. Mariam Kitosi – Times FM
5.Ergon Elly – Mbeya Highlands FM

2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
1. The Hitlist – Choice FM
2. Xxl – Clouds FM
3. Amplifaya – Clouds FM
4. Hatua Tatu – Times FM
5. Power Breakfast- Clouds FM

3. MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
1. Salama Jabir - EATV
2. Sam Misago - EATV
3. Zamaradi Mketema- Clouds TV
4. Salim Kikeke – BBC Swahili
5. Gondwin Gondwe – ITV

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
1. Friday Night Live – EATV
2. Mkasi – EATV
3. Planet Bongo - EATV
4. Uswazi - EATV
5. Take One – Clouds TV

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
1. Juma Kaseja – Yanga
2. Mrisho Ngassa – Yanga
3. Mbwana Samatta – TP Mazembe
4. Ramadhan Singano – Simba SC
5. Francis Cheka

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
1. Nisher
2. Adam Juma
3. Nick Dizzo
4. Mecky Kaloka
5. Jerry Mushala

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
1. My Number - Diamond
2. Jikubali – Ben Pol
3. Mirror – Baby
4. Love Me - Izzo Bizness f/ Barnaba & Shaa
5. Muziki Gani - Nay wa Mitego f/ Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
1. Amani ya Moyo – Feza Kessy
2. Closer – Vanessa Mdee
3. Sugua Gaga – Shaa
4. Yahaya – Lady Jaydee
5. Nakomaa na JIJI - Shilole

9. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Elizabeth ‘Lulu’ Michael
2. Jacqueline Wolper
3. Shamsa Ford
4. Irene Uwoya
5. Wastara Juma

10. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Jacob Stephen aka JB
2. King Majuto
3. Vincent ‘Ray’ Kigosi
4. Hemedy Suleiman
5. Salim ‘Gabo’ Ahmed

11. FILAMU INAYOPENDWA
1. Foolish Age – Elizabeth Michael
2. Bado Natafuta – Salim Ahmed, Shamsa Ford
3. Shikamoo Mzee – JB, Shamsa Ford, Majuto
4. Ndoa Yangu – Kanumba, Wolper
5. Zawadi Yangu – JB, Irene Uwoya

Akizungumzia tuzo hizo, meneja habari wa Bongo5, Fredrick Bundala amesema,"Upigaji kura utaendelea na sasa utajikita tu katika orodha ya majina haya matano, yaliyotangazwa kuongoza kwa kura, kwenye kila kipengele kinachoshindanishwa".

Wiki moja baada ya majina ya washiriki watano kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na kati ya wanaowania, mmoja ataondolewa na kubakiza wanne.

Wiki moja baada ya mchujo huo wa kwanza, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza wanaowania watatu kwenye kila kipengele.

Wanaowania tuzo wote (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa pili na (wa mwisho), watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki mbili baada ya mchujo huo wa pili, ili kutoa nafasi ya mashabiki wao kuendelea kupiga kura.”

Tunawaomba WaTanzania waendelee kuwapiga kura kupitia tovuti yetu, www.tuzozetu.com na pia kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno TUZOkwenda 15678 na baadaye kufuata maelekezo rahisi ya kupiga kura, alisema Fred.
  
KUHUSU TUZO ZA WATU 2014
Tuzo za watu Tanzania ni tuzo za aina yake, zilizoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini mahsusi kwaajili ya kuwapa mashabiki wa muziki, filamu, michezo na burudani, jukwaa huru kuwachagua wanaowapenda na kuwakubali katika vipengele vinavyoainishwa na tuzo hizi.

Tuzo hizi zitakazokua za kwanza kwa mwaka 2014, zinatarajiwa kuendeshwa kila mwaka.
Tuzo za watu zinalenga kuanzisha mchakato wa wazi  na huru wa utambuzi wa watu wenye umuhimu na michango mahsusi katika nyanja mbalimbali,wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe. Tuzo hizi  zitatumika kuanzisha urithi utakaoleta hatua mpya ya heshima kwenye jamii yetu

No comments:

Post a Comment