Pages

Wednesday, May 21, 2014

Jeshi la Kenya lawashambulia Alshabaab



Wanajeshi wa Kenya wanaendelea kukabiliana na Al Shabaab Somalia
Jeshi la Kenya limeishambulia ngome ya Al Shabab ya Jilib huko Somalia.
Katika mahojiano na BBC, msemaji wa Jeshi la Kenya Willy Wesonga amesema kuwa oparesheni hiyo kutoka angani imefaulu kuwaangamiza baadhi ya wakuu wa Al Shabab.
Ngome hiyo inadaiwa kuwa eneo ambapo wapiganaji hao wa kiislamu wanafanya mazoezi na mikutano yao.
Kikosi cha Kenya kinadai kuishambulia ngome hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wakaazi wa wilaya hiyo ya Jilib.
Wapiganaji wa Al shabab wamezidisha mashambulio nchini Kenya tangu nchi hiyo iingize wanajeshi wake ndani ya Somalia kuwasaka wapiganaji hao haramu mwaka wa 2011
Wesonga anasema jeshi la Kenya linalishambulia Al shabaab kama sehemu ya vita vikuu duniani dhidi ya ugaidi, na pia kuwazuia wafuasi wa kundi hilo kutekeleza mipango yao, yanayohatarisha usalama wa kieneo.
Hayo yanajiri wakati kundi la Al Shabab likidai kufanya shambulizi huko Mandera na kuwaua maafisa wa usalama wa Kenya.

No comments:

Post a Comment