Pages

Thursday, May 8, 2014

HESLB WAFUNGUA MAOMBI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA




Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imefungua maombi ya mikopo kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na Taasisi za Elimu ya Juu zinazotambulika, kwa masomo ya shahada mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2014/2015.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema maombi ya mikopo yanafanyika kwa njia ya mtandao (OLAS) yamefunguliwa kuanzia Aprili 23 na yatafungwa rasmi Juni 30, 2014.
Mwaisobwa alisema kuwa Bodi inatarajia kutoa mikopo kwa wanafunzi takriban 35,000 wa mwaka wa kwanza, watakaodahiliwa kujiunga na masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.

No comments:

Post a Comment