Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez ameumia goti akiwa mazoezini na ushiriki wake kwenye Kombe la Dunia uko mashakani. Striker huyo wa Liverpool atafanyiwa upasuaji mdogo leo. Kupona jeraha kama hilo huchukua kati ya siku 15 hadi 20. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uruguay. Suarez alimaliza msimu wa EPL kama mfungaji bora baada ya kupachika mabao 31.
No comments:
Post a Comment