Pages

Thursday, May 22, 2014

MWENYEKITI WA ARSENAL AMPA KICHWA NA JEURI WENGER,ASEMA ATALETA MAKOMBE MENGI

Confident: Arsenal chairman Sir Chips Keswick (left) is confident Arsene Wenger can deliver more trophies

Kaaminiwa: Mwenyekiti wa Arsenal,  Sir Chips Keswick (kushoto) anaamini  Arsene Wenger atawapatia makombe mengi zaidi. 
 MWENYEKITI wa Arsenal, Sir Chips Keswick anaamini kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Mfaransa Asernal Wnger muda si mrefu ataleta makombe mengi Emirates baada ya kubeba ndoo ya FA.
Muda wowote kutoka sasa, Asernal wanatarajia kutangaza kuongeza mkataba na Wenger kwasababu kocha huyo mwenye miaka 64 anajiandaa kwenda Brazil ambapo atakuwa mchambuzi wa kombe la dunia katika televisheni ya Ufaransa.
 Keswick alisema : 'nina matumaini kuwa ataendelea kufanikiwa zaidi na mafanikio yanakuja siku si nyingi. Tumeongeza kombe moja na tunahitaji mengine zaidi" 


Long wait: Wenger ended a nine-year wait for a trophy bu winning the FA Cup last weekend
'Mtu anayefanya kazi kama yeye, anastahili mafanikio yote yanayokuja katika njia zake. Amefanikiwa na kamwe sijawahi kuona mtu kama yeye,'  aliongeza Keswick kwenye mtandao wa klabu.
Wenger ameahidiwa paundi milioni 100 ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuwania taji la ligi kuu soka nchini England msimu ujao.

No comments:

Post a Comment