Pages

Friday, May 23, 2014

MAMA WA MIAKA 50 AJIFUNGUA WATOTO WA AJABU HUKO HANDENI TANGA

Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa na wanawake walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo waliotokana na teknolojia ya upandikizaji.
Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.
Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na wanawake wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na si kwa teknolojia ya upandikizaji.
Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13.

Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi anasimulia mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu aliyemzaa.
 
Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi wa Kata ya Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito, lakini walishangazwa na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza kumfanyia uchunguzi.

Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra sound (kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake.
 
Anasema baada ya kugundua kuwa hawataweza kumsafirisha kutokana na hali yake, ilibidi wamuweke katika ulisimamizi maalumu hadi siku ya kujifungua. Alijifungua kwa njia ya upasuaji.
 
Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5.

Anafafanua kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa hakuwa wa kawaida, alikuwa anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji na saa moja baadaye alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku moja na akafariki.

“Alikuwa na kilo sita pia alikuwa amevimba sana. Huu ni uzito mkubwa sana kwa mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka maji hadi mwili ukapungua kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea kuishi kwa saa 24,” anasema Dk Mushi.

 
Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili, lakini iliyoungana na kichwa chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa mbali. Hana kiuno wala mikono.

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment