Mheshimiwa
Ummy Mwalimu alipopata nafasi ya kwenda kumtembelea hospitali shosti yake,
Vicky Kamata.
Na
Mwandishi Wetu, Dar.
Sakata
la Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita Vicky Kamata sasa
limeingia katika ukurasa mpya baada ya kuzinduka na kuanza kulilia ndoa yake
huku nako wabunge mjini Dodoma wakililia michango yao.
Kwa
mujibu wa paparazi wetu aliyefika hospitali alipolazwa mbunge huyo ili aweze
kujua hali inavyokwenda na wananchi wanazungumzia suala hilo, alidadavua kuwa
kwa sasa Mbunge huyo amekuwa akililia ndoa yake.
"Yani
kila mmoja anaongea lake kuhusiana na sakata hili ila nimeweza kuongea na ndugu
wa karibu anasema kwa sasa ndugu yao analilia ndoa yake japo sisi tumesema
hatutaki hata kumuona tena huyo mwanaume anayeitwa Charles maana ndiye chanzo
cha yote haya yaliyotokea," alisema ndugu wa karibu wa Mheshimiwa Vicky
huku asitake kutajwa jina lake.
Wananchi
waliongeza kuwa hili lililomtokea mheshimiwa huyo ni dogo tu kufuatana na mambo
ambayo amekuwa akiyafanya, "Sisi Wananchi tunaamini kila unalolifanya
duniani malipo yake ni hapa hapa duniani hakuna haja ya kuficha ficha mambo...
huyu mheshimiwa amezidi kubeba beba waume za watu na inafikia mpaka anavunja
ndoa sasa hili lililomkuta ni fundisho kwake, ona sasa alivyoumbuka aibu hii
ataipeleka wapi??? wananchi hao walihoji huku wakisema hilo ni fundisho kwa
wote wenye tabia kama ya kwake.
HUKO
DODOMA:
Pamoja
na yote yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge waliochanga
pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza kuulizia michango yao
wataipataje kwa vile harusi basi tena!
“Huku
Dom (Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia michango
yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema mbunge mmoja
akiomba kuhifadhiwa jina.
Ndoa
ya Mheshimwa Vicky Kamata na Charles ilikuwa ifungwe Mei 24, 2014 katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar haikuweza
kufungwa kutokana na kuwekewa pingamizi kuwa muoaji alikuwa ni Mume wa Mama
Mwenye watoto 2.
No comments:
Post a Comment