Mwili
wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo
Mwili
wa Marehemu Munuo ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
wilaya ya Kahama
Mtumishi
wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa kahama, Mkoani Shinyanga,
Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya kulala
wageni mjini Kahama.
Taarifa
kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku
wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge iliyopo jirani na ofisi za
Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Taarifa
zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya saa 6 mchana baada
ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.
Jesh
la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na kumkuta marehemu
Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika halmashauri hiyo
akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu nne za mkononi.
Mwili
wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.
via>>>farajimfinanga.com
No comments:
Post a Comment