Pages

Wednesday, May 14, 2014

MLIPUKO WAUA 200 UTURUKI


Mmoja wa majeruhi akitolewa eneo la tukio.
MLIPUKO katika mgodi wa makaa ya mawe nchini Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 200 na kujeruhi wengine kadhaa.
Mlipuko huo umetokea jana katika mji wa Soma mkoa wa Manisa.
Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa na kifusi chini ya mgodi.
Wakati mlipuko huo ulipotokea, wafanyakazi 580 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia sehemu salama.

No comments:

Post a Comment