Stori: Musa Mateja
HOMA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, wamekumbwa na ugonjwa huo, habari zimefika katika dawati la Risasi Mchanganyiko.
“Nimeshitushwa sana na ugonjwa huu, maana katika maisha yangu ugonjwa ambao nilishawahi kuona unasumbua watu wa sehemu moja kwa wingi kiasi hiki ni Kipindupindu tu, sasa hii dengue ni hatari,” alisema Rehani na kuongeza kuwa wanamuziki hao walikuwa wamelazwa Hospitali ya Mwananyamala na kwamba hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.
Naye mmoja wa wagonjwa hao, Rama Pentagoni, alipozungumza na mwandishi wetu alisema anaendelea vizuri, huku akiuelezea ugonjwa huo kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu.chanzo GPL
No comments:
Post a Comment