Kaaminiwa: Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick (kushoto) anaamini Arsene Wenger atawapatia makombe mengi zaidi.
MWENYEKITI wa Arsenal, Sir Chips Keswick anaamini kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Mfaransa Asernal Wnger muda si mrefu ataleta makombe mengi Emirates baada ya kubeba ndoo ya FA.
Muda wowote kutoka sasa, Asernal wanatarajia kutangaza kuongeza mkataba na Wenger kwasababu kocha huyo mwenye miaka 64 anajiandaa kwenda Brazil ambapo atakuwa mchambuzi wa kombe la dunia katika televisheni ya Ufaransa.
'Mtu anayefanya kazi kama yeye, anastahili mafanikio yote yanayokuja katika njia zake. Amefanikiwa na kamwe sijawahi kuona mtu kama yeye,' aliongeza Keswick kwenye mtandao wa klabu.
Wenger ameahidiwa paundi milioni 100 ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuwania taji la ligi kuu soka nchini England msimu ujao.
No comments:
Post a Comment