Baada ya time ya Babu wa Loliondo kuponya kwa kutumia kikombe,sasa ni time ya kiongozi wa dini ambaye anajiita nabii na kutangaza kuwa anatibu ugonjwa wa Dengue kwa kutumia juisi.
Nabii huyu anayejulikana kwa jina la Yaspi Bendera baada ya taarifa zake kusambaa kumefanya baadhi ya wagonjwa kuanza kwenda kwenye kanisa lake la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo Yombo Buza-Kipera.
Ingawa Serikali imeonya vitendo vya baadhi ya watu kuwaondoa wagonjwa hospitalini na kuwapeleka kwenye maombi na kusema mtu yeyote anayesababisha wagonjwa kuondolewa hospitalini kwenda kufanyiwa maombi atachukuliwa kuwa ni adui namba moja,katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa
Taarifa ya wataalam inasema kuwa ugonjwa huo unatokana na mbu aina ya aedes egypti sasa Nabii Yaspi anadai kuwa homa ya dengue ni pigo lililoletwa na Mungu kwa watu wasiotaka kumtii.
Nabii huyo anadai kuwa alionyeshwa na Mungu miezi miwili iliyopita kuwa homa ya ugonjwa huo ingeibuka nchini na kwamba itawaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto.
Nambii huyo kasema kuwa moyoni ana siri nzito ambayo atamwambia mkuu wa nchi peke yake ambaye ni Rais Jakaya Kikwete na endapo atakosa nafasi ya kufanya hivyo hatamwambia mtu mwingine.
-millard ayo
No comments:
Post a Comment