Serikali imetangaza kupunguza bei ya Umeme nchini ndani ya miezi sita baada ya bomba la gesi kukamilika. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Steven Masele.
Masele amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Bomba la gesi na gesi kuanza kutumika, serikali itauza umeme kwa senti nane hadi tisa kutoka bei ya sasa ya senti 35 hadi 40.

Amesema hatua hiyo ya serikali itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unatokana na ukataji wa miti holela kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Hatua ya kupunguza bei ya Umeme itaenda sambamba na kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Huduma za utumiaji wa Umeme kwa bei rahisi na kuachana na matumizi ya nishati ya mkaa.

Pamoja na mpango huo wa serikali pia kupitia TANAPA na World Wildlife Fund (WWF) ilifanya maandalizi ya upatikanaji wa nishati mbadala kwa kipindi cha miaka 10, ikiwemo kuwapatia wananchi miche ya miti bure.

Miche ambayo wananchi watapanda kwenye mashamba yao ili kupata kuni.