JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
UTANGULIZI
Mnamo tarehe 27 Januari 2014, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya dengue katika Kliniki ya ‘International School of Tanganyika’ iliyopo Manispaa ya Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam. Taarifa hiyo ya awali ilionyesha kuwepo kwa jumla ya wagonjwa 6 katika kituo hicho bila vifo.
Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na
- UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes. Dalili za ugonjwa huu ni homa ya ghafla,mwili kuchoka, kuumwa na viungo, kuvimba tezi na kupatwa na harara. Uwepo wa homa, kuumwa kichwa maumivu ya viungo na uchovu ndio dalili kuu za ugonjwa huu. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukiwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria. Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;
Aina ya pili na ya tatu ni aina zenye dalili mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa na hatimaye kusababisha kifo. Kwa Tanzania, hadi sasa ni aina ya kwanza ya Homa ya Dengue imeripotiwa.
Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina ya “Aedes”. Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.
Ugonjwa huu hauenezwi moja kwa moja kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine bali kwa kupitia mbu aliyeambukizwa na virusi vya homa ya dengue anapomuuma binadamu. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna tiba maalum ya kutibu virusi vya denge wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue:
*Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
* Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
* Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo yaharuhusu maji kutuma
* Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
*Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
o Kujikinga na kuumwa na mbu
* Tumia dawa za kufukuza mbu “mosquito repellants”
* Vaa nguo ndefu
* Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (hasa kwa wale wanalala majira ya mchana)
* Weka wavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
2. HALI HALISI YA SASA YA UGONJWA NCHINI
11.1 Idadi ya Wagonjwa:
Kuanzia tarehe 27 Januari hadi tarehe 6 April 2014, jumla ya wagonjwa 399 (Kinondoni – 322, Ilala – 61 na Temeke – 16) wamethibitishwa kuwa na ugonjwa homa ya dengue. kati yao, wagonjwa wawili (2) wamepoteza maisha;
(i) Mwanamke, umri miaka 22, aliyefariki katika Hospitali ya Mwananyamala tarehe 14.3.2014.
(ii) Mwanamke, umri miaka 37, muuguzi, aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Temeke ambaye alifia hospitali ya MNH
11.2 Maeneo yaliyoathirika
Ugonjwa huu umeripotiwa katika kila eneo la Dar es salaam lakini Kata zilizoathirika zaidi kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi ni kama zifuatatazo;
KATA |
IDADI
|
Msasani |
93
|
Masaki |
68
|
Magomeni |
54
|
Kinondoni A/B/Manyanya |
29
|
Mikocheni |
21
|
Buguruni |
20
|
Tandale |
15
|
Sinza/Kijitonyama |
13
|
11.3 Dalili za kuu zilizojitokeza
Wagonjwa wote 399 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa walikuwa na na homa kali.. Aidha 82% ya wagonjwa walionyesha pia dalli ya kuumwa kichwa. Dalili nyingine ni zilizojitokeza ni pamoja na kutapika, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, na kuumwa tumbo.
11.4 Jinsia na Umri
Kati ya Wagonjwa 376, 214 (54%) walikuwa wanaume na 185(46%) walikuwa ni wanawake. Idadi kubwa ya wagonjwa waliothibitika kuwa na ugonjwa huu wako katika Umri zaidi ya miaka 16 yaani asilimia 92. Aidha watoto chini ya umri wa miaka 5 walikuwa ni asilimia 2 tu.
Mlipuko huu wa tatu wa dengue hapa nchini ulianza tarehe 2 Januari 2014. Ongezeko kubwa la wagonjwa limejitokeza katika mwezi wa tatu (3) mwishoni na kushika kasi mwezi wa Aprili, 2014 ambapo wagonjwa wengi wameongezeka.
Jedwali No 1: Mwenendo wa Ugonjwa wa Dengue kuanzia utokee,2 Januari 2014- 6 May 2014 (N=399)
- HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA WIZARA
*WAUJ imetoa tamko la Serikali kwa wananchi kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye vyombo vya habari
tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014. Aidha, uelimishaji kwa wananchi
unaendelea kupitia Radio, TV na magazeti. Aidha matumizi ya Vipaza sauti katika
ngazi za chini utaanza na kusimamiwa na Halmashauri za Wilaya mkoani Dar es
salaam.
*Kuendelea kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga
Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia
inajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),
“Ukweli Kuhusu Ugonjwa“(Fact sheet) na mwongozo wa uchukuaji wa sampuli
na matibabu.
* Kuendelea kutoa elimu kwa Watumishi wa afya madaktari pamoja na
wanaofanya maabara kuhusu namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha
watumishi wa hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke
wamekwisha kupewa mafunzo haya na bado yanaendelea kutolewa kupitia
mikutano ya kila asubuhi ya kiltaaluma (Clinical meetings). Halmashauri
zinaendelea pia kuyatoa mafunzo haya katika ngazi za chini.
*Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu.
Kuanzishwa kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika
Hospitali za Manispaa za jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na
Temeke Hospitali), aidha, Kituo cha ‘ International School of Tanganyika – IST’
kilichopo Manispaa ya Kinondoni pia kinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu
pamoja na Kituo cha Hospital ya Muhimbili.
*Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya
Taifa (NHLQATC) ambapo mpaka sasa kumethibitishwa kuwepo kwa aina 2 za
virusi hivi yaani DENV2 na DENV3. Vile vile Wizara imepeleka kiasi kidogocha
vipimo vya awali yaani “Dengue Rapid Test Kits” kwa baadhi ya vituo vya Dar
es salaam kuimarisha utambuzi na vituo hivo ni pamoja na Muhimbili, Amana
hospital, Mwananyamala hospitali, Temeke Hospital, na IST kliniki.
*Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa
(saveilensi) ya IDSR . Aidha, Wizara imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu
wa mikoa na wilaya kutoa taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa
za kila wiki (Infectious disease week ending).
*Kutoa miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani
kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri
anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi
wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
Kudhibiti mbu kwa kupulizia dawa ( Fogging) katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam. Aidha mpango wa WAUJ ni kufikia maeneo mengi zaidi pamoja na kufanya kuweka dawa ya kuua viliwi luwi (Larviciding)” kwa viluwiluwi.
*Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama
mwongozo wa Kimataifa uvyaoelekeza.
* Kupitia Timu ya Taifa ya Maafa, Wizara imeandaa mpango kazi na mkakati
wa muda mfupi wa namna ambavyo ugonjwa huu utadhibitiwa ukishirikisha
wadau mbalimbali. Kimabatanisho namba 1 kinafafanua kazi zilizoaninishwa.
3.2 Hatua za muda mrefu
* WAUJ imeandaa Mpango Mkakati (2014 – 2018) wa kukabiliana na magonjwa ya ‘Viral Haemerrhagic Fevers’ ikihusisha na ugonjwa wa homa ya dengue.* Halmashauri za mkoa kutengeneza “strategic plan” ya kwao kwa kuangalia “prototype plan” ya WAUJ
- Changamoto
MAAZIMIO YA KIKAO CHA TIMU YA TAIFA YA MAAFA KUHUSUIANA NA DENGUE FEVER
TAREHE 7.5.2014
Kazi
|
Shughuli
|
Mhusika
|
Muda wa Utekelezaji
|
Uratibu wa shughuli za Dengue Kitaifa
|
Kuwasilisha mpango kazi ulioandaliwa kwa ngazi za juu ili pia uweze kuwasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu
|
WAUJ: Epidemiolojia
|
Mara moja
|
Uratibu wa shughuli za Dengue mkoani Dar es salaam
|
Kuandaa mpango mkakati wa namna ya kukabiliana na Dengue kwa kutumia prototype plan ya mpango mkakati wa Kitaifa
|
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Tarehe 12.5.2014
|
Udhibiti wa Mbu na viluwiluwi
|
Kuua mazalio ya mbu yaani viluwili (Larvidicing) kwa kutumia bio-larvicide –ambao iko kwa kiasi iliyokuwa inatumika katika mradi wa Bio larvicide kati ya Cuba na WAUJ kupitia NMCP. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
Kuendelea na kufanya fogging (kuua mbu wapevu) wenye tayari vimelea kutumia viautilifu vya kuua mbu katika maeneo yaliyotoka idadi ya wagonjwa wengi. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
|
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara moja (Angalizo: utategemea pia hali ya hewa na mvua)
|
: Maafisa Afya wote wa Halmashauri watahusika katika kusimamia na kuhamasisha usafi wa mazingira kwa kutumia sheria ndogo ndogo ilizojiwekea ikiwemo na kutoa faini
|
WAUJ: Kitengo cha Usafi wa Mazingira
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara moja
| |
Maafisa Afya ikiwemo wa kata wataelemisha wananchi namna ya kudhibiti ugonjwa kwa vipaza sauti, uongozi wa mitaa, kugawa vielemishi. Na vilevile kuendelea kutumia vyombo vya habari na TV
|
WAUJ: Kitengo cha Usafi cha mazingira na Elimu ya Afya
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
| ||
Elimu kwa watumishi wa Afya
|
Kutoa elimu kupitia clinical meetings katika hospitali zote za wilaya na pia kupitia APHTA
|
WAUJ: Epidemiolojia
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara moja
|
Kuimarisha utambuzi wa ugonjwa
|
WAUJ kuwasiliana na MSD kuhusu upatikanaji wa “Dengue Rapid Kits” ili Halmashauri ziweze kufuata utaratibu wa manunuzi
Halmashauri na pia MNH kupanga katika mipango yao fedha za kununua kits hizi
Kwa kipindi hiki ambapo “kits” zinaonekana kupungua katika maeneo tajwa yaani MNH, na Hospital za Wilaya mkoani Dar es salaam, NHLQATC itatumika kupima vipimo hivi ili kuwepo na mwenendelezo wa “Sentinel Surveillance”
|
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara moja
|
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa
|
Kutengeneza protocol ya Surveillance pamoja na alogarithm ya matibabu
|
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
|
10.5.2014
|
Kuweka “messages” katika Point of Entry
|
WAUJ: Kitengo cha Afya ya Mazingira
|
Mara moja
| |
Ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu
|
WAUJ kuandika barua kwa RAS Dar es saalam kuanisha maeneo ya utekelezaji ambao yako chini ya mamlaka yake
WAUJ kuandika barua ya kuomba zaidi msaada wa “Dengue Rapid Kits” WHO, CDC na USAID
|
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
|
Mara moja
|
UNICEF kusaidia na IEC materials yaani Posters na leaflets ambazo tayari zimeshatengenezwa
|
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
|
Mara moja maana tayari kuna mawasiliano
| |
WHO kusaidia katika uelimishaji kwa kupitia kifungu cha fedha za “World Health Day” iliyolenga masuala ya “vector”
|
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
|
Utekelezaji unategemea barua kuandikwa kutoka WAUJ kwenda WHO
|
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Epidemiolojia na Ufuatiliaji wa Magonjwa
May, 2014
No comments:
Post a Comment