Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC, Dk Damas ndumbaro kulia akifafanua jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo. Kushoto ni Katibu wa Kamati, Issa Batenga |
Na Mahmoud Zubeiry,
KAMA ilivyotarajiwa, Michael Richard
Wambura ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi mkuu wa Simba SC
unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao, kwa sababu kubwa mbili.
Akizungumza katika Mkutano maalum na
Waandishi wa Habari mchana huu makao makuu ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), makutano ya mitaa ya Ohio na Libya, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC, Wakili Dk Damas Daniel
Ndumbaro amesema Wambura ameondolewa kwa sababu kwa sasa si mwanachama
halali wa klabu hiyo.
Wambura
alisimamishwa uanachama wa Klabu ya Simba tangu Mei 5 mwaka 2010
kutokana na kosa la kuipeleka klabu hiyo mahakamani akifungua kesi namba
100 ya mwaka 2010 katika Mahakama ya Kisutu mjini Dar es Salaam.Ndumbaro
amesema kuwa Wambura aliwasilisha barua pia katika Kamati ya Uchaguzi
akikiri kuipeleka Simba mahakamani na kuiomba Kamati hiyo kumaliza suala
lake na kuahidi hatarudia tena kufanya kosa kama hilo, amepingana na
Katiba ya klabu, TFF na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Mwenyekiti huyo wa Kamati amesema kwamba pia walipokea barua mbili
tofauti kutoka kwa Wambura ya kwanza ikiwa ya Novemba 6 mwaka 2012 mgombea huyo akitaka kujua uhalali wa uanachama wake na nyingine ya Septemba 15 ikijibu kuwa Simba haina tatizo lolote na yeye.
tofauti kutoka kwa Wambura ya kwanza ikiwa ya Novemba 6 mwaka 2012 mgombea huyo akitaka kujua uhalali wa uanachama wake na nyingine ya Septemba 15 ikijibu kuwa Simba haina tatizo lolote na yeye.
“Kuna utata katika barua zake na pia kuna barua ya tatu ya Septemba 25
mwaka 2012 ikieleza pia Simba hawana tatizo na Wambura,” amesema
Ndumbaro.
Aliongeza kuwa kutokana na Kamati yake kujiridhisha na maelezo hayo,
imeamua kumuondoa Wambura katika kinyang’anyiro cha uchaguzi.
Ndumbaro ameeleza zaidi kuwa kutokana na maamuzi ya kusimamishwa huko,
Wambura hapaswi kushiriki katika shughuli za Simba kwa mujibu wa Ibara
ya 12(3) ya katiba ya klabu hiyo ya mwaka 2010 na ibara ya 12(3) ya
2014.
Alieleza kuwa endapoa Wambura hataridhika na maamuzi hayo anaruhusiwa kukata rufaa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF.
Ndumbaro amesema pia wagombea wengine wote walioekewa pingamizi
wamepitishwa na wataendelea na mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika
Juni 29 mwaka huu.
Kwa kuondolewa Wambura, nafasi ya wagombea Urais inabaki na watu wawili,
ambao ni Evans Elieza Aveva na Andrew Peter Tupa, wakati wanaowania
Umakamu wa Rais ni Jamhuri Kihwelo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Joseph
Itang’are ‘Kinesi’ na Swedi Nkwabi.
Alipotafutwa
kuzungumzia suala hilo, Wambura amesema kwamba atazungumza kesho katika
Mkutano na Waandishi wa Habari, kwa leo hakuwa tayari kuzungumza na mtu
mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment