Bibi
wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani.
BIBI
wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa kizimbani kwa ajili
ya kusomewa kesi yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 37.
Hakimu
aliyepelekewa kesi hiyo, Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili
bibi huyo ambaye hajui Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.
Cole
alisema lugha anayoweza kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini
Nigeria. Katika hali iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio
akiomba Mungu amsaidie.
No comments:
Post a Comment