Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke
Askari polisi mmoja wa kituo cha
polisi Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa Temeke, ameuawa kikatili siku ya ijumaa
mchana baada ya kupigwa risasi ya kifua na majambazi waliokuwa wanajaribu
kutoroka baada ya kufanya tukio la kihalifu. Askari hao waliokuwa doria katika
eneo la Wailes walijikuta wakishambuliwa kwa risasi na majambazi hao mara baada
ya majambazi hao kujaribu kukimbia katika eneo la tukio kwa kutumia usafiri wa
pikipiki kipindi ambapo askari polisi walikuwa karibu na eneo la tukio. Hata
hivyo wakati askari hao wakijaribu kuwafukuza majambazi hao wawili kwa lengo la
kuwakamata ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na kumpiga risasi ya kifua askari
huyo na kufariki pale pale.
Mwili wa askari huyo ukiwa
umehifadhiwa.
Hata hivyo katika harakati za
kujaribu kukimbia majambazi hao walianguka na pikipiki waliyokuwa wakitumia
ndipo wakaamua kutimua mbio mitaani na kuingia katika nyumba moja ambapo
walijificha na kujifanya kama ni wakazi wa eneo hilo, baada ya wnanchi na
polisi kufika katika nyumba hiyo, baadhi ya majirani waliwaambia polisi kwamba
wameona watu hao wameingia katika nyumba hiyo. Baada ya polisi kuingia
waliwakuta watu hao wakiwa wametulia kama kwamba wao ni wakaazi wa nyumba hiyo
na wala hawajui lililotokea.
Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa
chumba cha kuhifadhia maiti
Baada ya kuwatambua watu hao, polisi
waliwatia nguvuni huku wananchi wenye ghadhabu waking'ang'ania kuwa wanataka
kuwaua sababu wameshaua askari mmoja. Baada ya vuta nikuvute kati ya wananchi
na askari hao ambao walikuwa wachache, wananchi walifanikiwa kuwachukua
majambazi hao kwa nguvu kutoka mikononi mwa polisi na kuanza kuwapiga kwa
silaha mbalimbali za kienyeji yakiwemo mawe na marungu mpaka watuhumiwa hao
wakapoteza maisha.
Mwili wa jambazi mwingine ukiwa
umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Mwili wa askari polisi ukiwa
umepakiwa kwenye gari ya polisi tayari kupelekwa hospitali ya Temeke
kuhifadhiwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
waliiambia blogu hii kwamba majambazi hayo kabla ya kupambana na polisi
walikuwa wamefanya uvamizi na kumuibia mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo. Hata
hivyo mali au fedha iliyoibiwa haikuweza kujulikana mara moja.
dawa ya moto ni moto wananchi wamefanya jambo poa maana haiwezekani waue askari alafu wakake sege dance wale ugali wa bure na wao wakakutane na huyo askari huko mbele kwa mbele wapewe hukumu... Askari mmoja ni sawa na raia 50 commando mmoja ni sawa na raia 100
ReplyDelete