Wapiga kura kwenye foleni
Wake wa meya wawili wa upinzani
waotumikia kifungo cha jela nchini Venezuela wameshinda uchaguzi na kuwarithi
waume zao.
Wanawake hao, Patricia Gutierrez na
Rosa Brandonisio walishindwa kwa asilimia 73 ya kura katika mji wa San
Cristobal na asilimia 88 ya kura katika mji wa San Diego mtawalia.
Waume zao Daniel Ceballos na Vicencio Scarano,
walihukumiwa vifungo vya mwaka mmoja na miezi kumi mtawalia baada ya kupatikana
na hatia ya kukosa kuondoa vizuizi ambavyo vilikuwa vimewekwa na wafuasi wao
barabarani
Patricia Gutierrez akiwa na wanawe
Wanasiasa hao walifungwa jela mapema
mwaka huu
Ushindi wa wanawake hao umepongezwa
hata na baadhi ya wanasiasa kutoka chama tawala huku wakisema liwe funzo kwa
wanasiasa wengine.
Venezuela imekuwa ikikumbwa na
maandamano makubwa ya kupinga serikali tangu mwezi Februari.
Mazungumzo kati ya serikali na
upinzani kusuluhisha mgogoro huo yamekwama kwa sasa.
Rosa Brandonisio (Katikati)
San Cristobal na San Diego ni ngome
za upinzani na usihindi wa wanawake hao, sio jambo la kushangaza sana.
Lakini wadadisi wanasema ushindi wao
utaimarisha upinzani dhidi ya chama tawala.
Miji hiyo miwili imeshuhudia vurugu
mbaya zaidi ambapo watu 42 waliuawa kutoka pande zote mbili.
Maandamano yalianza baada ya
wanafunzi kulalamikia kile walichosema ni ukosefu wa usalama.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment