Pages

Tuesday, May 27, 2014

Wake wa Meya walio jela washinda uchaguzi


Wapiga kura kwenye foleni
Wake wa meya wawili wa upinzani waotumikia kifungo cha jela nchini Venezuela wameshinda uchaguzi na kuwarithi waume zao.
Wanawake hao, Patricia Gutierrez na Rosa Brandonisio walishindwa kwa asilimia 73 ya kura katika mji wa San Cristobal na asilimia 88 ya kura katika mji wa San Diego mtawalia.
Waume zao Daniel Ceballos na Vicencio Scarano, walihukumiwa vifungo vya mwaka mmoja na miezi kumi mtawalia baada ya kupatikana na hatia ya kukosa kuondoa vizuizi ambavyo vilikuwa vimewekwa na wafuasi wao barabarani


Patricia Gutierrez akiwa na wanawe
Wanasiasa hao walifungwa jela mapema mwaka huu
Ushindi wa wanawake hao umepongezwa hata na baadhi ya wanasiasa kutoka chama tawala huku wakisema liwe funzo kwa wanasiasa wengine.
Venezuela imekuwa ikikumbwa na maandamano makubwa ya kupinga serikali tangu mwezi Februari.
Mazungumzo kati ya serikali na upinzani kusuluhisha mgogoro huo yamekwama kwa sasa.





Rosa Brandonisio (Katikati)
San Cristobal na San Diego ni ngome za upinzani na usihindi wa wanawake hao, sio jambo la kushangaza sana.
Lakini wadadisi wanasema ushindi wao utaimarisha upinzani dhidi ya chama tawala.
Miji hiyo miwili imeshuhudia vurugu mbaya zaidi ambapo watu 42 waliuawa kutoka pande zote mbili.
Maandamano yalianza baada ya wanafunzi kulalamikia kile walichosema ni ukosefu wa usalama.chanzo BBC

No comments:

Post a Comment