Marehemu Geofrey Ndibalema (41), mkazi wa Tandika jijini Dar
aliyejinyonga kwa kukosa kodi ya chumba.
Marehemu Geofrey Ndibalema (wa pili kulia) enzi za uhai
wake.
INASIKITISHA! Geofrey Ndibalema (41), mkazi wa Tandika
jijini Dar amedaiwa kujinyonga kwa kukosa kodi ya chumba.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Juni 14, mwaka huu
katika nyumba aliyopanga marehemu ambapo ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya
tukio, baba
mwenye nyumba alimpigia simu kumkumbushia akaahidi kulipa siku
iliyofuata ambayo ndiyo alikutwa amejinyonga.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu aliyeomba hifadhi
ya jina lake, alisema Geofrey aliamka asubuhi akiwa mzima wa afya na kwenda
kuchota maji ya kuoga ili aelekee kwenye shughuli zake za upambaji ambapo
ilidaiwa kuwa alipewa tenda ya kupamba katika harusi na tayari alishachukua
nusu ya malipo.
Ndugu huyo wa marehemu alidai, wakati Geofrey anarudi
kuchota maji, alimkuta mwenye nyumba akiwa anamsubiri ili alipe kodi yake jambo
lililodaiwa kumpa hofu marehemu na kuingia ndani ya chumba chake na kujinyonga.
No comments:
Post a Comment