Kiungo wa timu ya taifa ya Croatia Ivan Rakiti ameonyesha
kibweka mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa mzunguuko wa pili wa kundi la kwanza
dhidi timu ya Cameroon, ambayo ilikubali kufungwa mabao manne kwa sifuri.
RakitiÄ, ameonyesha kibweka hicho baada ya kubadilishana
jezi na bukta na aliyekuwa kiungo mwenzake katika klabu ya Sivilla, Stéphane
Mbia wakati wakielekea
kwenye vyumba vya kubadilishia.
Rakitic ambae amesajiliwa na FC Barcelona siku tatu
zilizopita alichojoa bukta yake na kubaki na nguo ya ndani ili hali Mbia
alionekana kujistiri kufuatia nguo ya kubana aliyobaki nayo mwilini.
Kitendo hicho kilifanyika mbele ya waandishi wa habari
pamoja na maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA.
No comments:
Post a Comment