Mgombea wa nafasi ya urais klabuni hapo, Michael Wambura.
RASMI Kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
imemrejeha Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura kwenye mbio za
kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amewaambia
Waandishi wa Habari mchana wa leo ofisi za TFF katikati ya Jiji la Dar es
Salaam, kwamba Wambura amerejeshwa baada ya kikao chao kilichodumu kwa siku
mbili.Baada ya mlolongo mrefu tangu juzi Saa 5:00 asubuhi hoteli ya Courtyad
,
Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya jana, Wajumbe wa Kamati hiyo waliamua
kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya tano za kumkubalia
aendelee na mbio za Urais Simba SC.
Ikumbukwe Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa
Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua katika kinyang’anyiro cha kuwania
urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi
huu.Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas
Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na
FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.
No comments:
Post a Comment