Pages

Tuesday, June 10, 2014

HUTAMSIKIA TENA DINA MARIOS WA LEO TENA REDIONI AWAAGA MASHABIKI WAKE



Wapenzi wangu najua kila kitu kilianzia kwenye leo tena hadi wewe kuamua kufatilia kazi zangu na kila kitu ninachofanya.Ila wanasema safari moja huanzisha nyingine ndivyo ilivyo kwangu.Baada ya muda wa miaka nane kuongoza leo tena na mie kuilea kwa kila hali kuhakikisha inakuwepo.Leo tena ilikuwa maisha yangu nikilala,nikiamka,nikiwa barabarani ili mradi niwe na jambo kwa msikilizaji wangu kila siku.Iwe ni segment mpya,topic,wimbo,jingle,yaani chochote ambacho naona kitanogesha kipindi. Nilichukua likizo ya martenity na niliporejea nikaambiwa dada tunakuhamishia 

 
sehemu nyingine,TV.Daah haikuwa kazi rahisi kukubali na kuipokea niliona daah itakuwaje jamani mbona leo tena ndio kila kitu kwangu. 

Nikaelezwa vile ofisi ina malengo makubwa na kipindi kipya nitakachoanzisha ambayo siwezi kuyaanika hapa lol basi kidogo kidogo nikaanza kuelewa somo na sasa nipo tayari.Kuna wale ambao bado mnaendelea kuulizia kwa nini hamnisikii ukweli ndio huo kwa sasa sipo tena kwenye leo tena najiandaa na kipindi changu kipya cha tv kitakachoruka clouds tv hapo baadae.Japo nina changamoto ya mwili mmenenepa mie ila kila kitu kitajiset mbele ya safati.Nikiwa najiandaa na kipindi kipya pia najiaandaa na ule utaratibu wangu wa kusaidia watoto yatima kupitia dada dina cares ambayo itakuwa ni mwezi ujao.Najua tayari nina mawazo yangu ya nini nitafanya kwenye hicho kipindi lakini pia naomba nikuulize.Ungependa kuona nini kwenye kipindi changu cha tv?

No comments:

Post a Comment