Pages

Tuesday, June 10, 2014

TP MAZEMBE YAICHAPA ZAMALEK 1-0 NA KUKALIA USUKANI WA KUNDI A

 
TP MAZEMBE jana imefanikiwa kuilaza bao 1-0 Zamalek SC ya Misri katika mchezo wa kundi A wa ligi ya mabingwa barani Afrika kwenye uwanja wa Mazembe, mjini Lubumbashi,  nchni DR Congo.
Bao hilo pekee lilifungwa na Mzambia Rainford Kalaba katika dakika ya 13 na matokeo hayo yanawafanya Mazembe kukalia usukani wa kundi A kwa pointi zao 6 walizokusanya katika mechi tatu.
Mechi mbili za kwanza, TP Mazembe ilifungwa bao 1-0 na Al Hilal ya Sudan na kushinda bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao, AS Vita mjini Lubumbashi.
Mechi nyingine jana iliwakutanisha AS Vita waliokuwa ugenini dhidi ya Al Hilal na timu hizo kutoka sare, hivyo kufungwana kwa kila kitu, kwa maana ya pointi nne na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. Kila timu imefunga magoli matatu na kufungwa matatu.
Wazoefu kutoka Misri, klabu ya Zamalek inaburuza mkia kwa pointi zake tatu.
Michuano hiyo itasimama kupisha kombe la dunia linaloanza kutimua vumbi juni 12 mwaka huu nchini Brazil na baada ya mashindano hayo kumalizika julai 13 ndipo mzunguko wa pili wa ligi ya mabingwa utaanza.

No comments:

Post a Comment