Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James
Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama hatua
ya kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga.Kwa mujibu wa BBC, Balozi Mugume
ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya
mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua
waliyochukua.Amesisitiza kuwa wataieleza
Marekani sheria hiyo inapinga tabiaambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika
jamii nyingi za
kiafrika.Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa
na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii ,kuwatayari
sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
No comments:
Post a Comment