Koplo wa polisi matatani eti sketi imembana
Koplo wa Kitengo cha Traffiki aliyepigwa picha akiwa
amevalia sketi iliyomabana makalio amelazimika kukimbilia mahakamani kuokoa
kazi yake.Linda Okello alikimbilia Mahakamani Baada ya wakubwa wake kutaka
kumchukulia hatua ya kinidhamu wakidai alikosa nidhamu ya kazi alipovalia sketi
iliyoonesha umbo lake akiwa kazini
Kinyume na kanuni za idara ya polisi ya mwaka wa 2011.
Dada huyo aliyezua mjadala kote duniani kuhusu wanawake
waliojaliwa makalio makubwa na kama wanabaguliwa kutokana na maumbile yao
amemshtaki Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya miongoni mwa tume inayosimamia
polisi nchini humo.
Koplo Linda anasema kuwa Afisa mkuu wa wilaya ya kiambu
Stephen Ngetich hata hakuwepo katika eneo la tukio lakini ndiye aliyemshmtaki.Linda
alipigwa picha akilinda usalama katika mashindano ya mbio za magari ya Kiambu
na picha hiyo ikaenea sana katika mitandao ya kijamii kuhusiano na urefu wake
na pia makalio na umbo lake
Sasa koplo huyo anaitaka mahakama ifutilie mbali kesi ilyoko dhidi yake akisema,kuwa anahisi ataonewa na wakubwa wake kutokana na majaliwa yake .
Aidha koplo huyo huyo anasema kuwa japo alipewa Suruali ndefu mbili iliasiivae tena sketi hiyo yake ,Koplo anadai kuwa bosi wake hakuwahi kumkaripia kwa kuivalia na kuwa madai dhidi yake yanashinikizwa tu na watu waliovutiwa na mjadala katika mitandao ya kijamii.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu.
Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana.
No comments:
Post a Comment