Katika mechi za kirafiki kwa maandalizi ya michuano ya kombe
la dunia, England ilitoka sare ya 2 - 2, dhidi ya Ecuador katika mechi
iliyochezwa huko Miami. Timu ya England iliongozwa na Frank Lampard.
Raheem Sterling ambaye huchezea kalbu Liverpool,
alibanduliwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 11 baada ya mtafaruku
kati yake na Antonio Valencia ambaye huchezea klabu ya Machester United.
Sterling amepigwa marufuku kushiriki mechi ya kirafiki
itakayofuata.
Ecuador iliikanda kanda England na kutumia fursa ya ulinzi
mbovu huku ambapo Enner Valencia aliwaongoza kushambulia awali lakini Wayne Rooney
akapata fursa ya kupenyeza bao lake la 39 kufaidi England kabla ya kwenda
mapumziko.
Sasa England itabidi kujipiga msasa wakijiandaa kwa mechi ya
kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Jumamozi kabl aya kusafiri kwenda Brazil
kuanza ngoma ya kupigania kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment