Shambulio limetokea katika jimbo la Yobe nchini Nigeria
wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia.Jimbo hilo limewekwa katika hali
ya hatari huku maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio
yanayofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.Wakaazi
wanasema walisikia sauti ya mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini
Damaturu ambapo mashabiki wa soka walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe
la dunia.
Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitolea mhanga
aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa katika jimbo la
Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea
Yobe imekumbwa na mashambulizi ya Boko Haram katika miaka
iliyopita.
Duru kutoka hospitalini zinasema malori kadhaa
yamewasafirisha majeruhi kupata matibabu na polisi wanasema maafisa wamepelekwa
katika eneo hilo.
Mfanyikazi mmoja wa hospitali ameaimbia BBC kuwa
waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na
mikono.Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo la Adamawa ambalo liko
katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika
katika maeneo ya umma kutazama mechi za kombe la dunia kutokana na hofu ya
Usalama.Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la
burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.
Hali ya hatari
Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya
tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila mara ya
wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram..
Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya
uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009.
No comments:
Post a Comment