Pages

Monday, June 23, 2014

NAPE: WASOMI CHANGIENI MAONI YENU KATIKA KUBORESHA SERA MBALI MBALI

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM wa Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM waliohitimu masomo yao katika Chuo cha SAUT ambapo aliwaambia wasomi washiriki katika kukisaidia chama hasa katika kuboresha sera mbali mbali.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akizungumza wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ,Mwenyekiti aliwaeleza wanafunzi hao kuwa CCM ni chama pekee kinachoweza kuwavusha kutoka hapa walipo na kusonga mbele.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ambapo alisisitiza wasomi kufanya tafiti zao kabla ya kuchagua chama gani cha siasa kinaweza kuwasaidia.


 Baadhi ya wanachama waliohitimu kutoka chuo cha SAUT wakifuatilia kwa makini hotuba kutoka kwa viongozi wao wakati wa sherehe za kuwaaga rasmi zilizofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste COCO Beach Mtwara
 Mwajuma Abas Nasombe na Zena Ibrahim wakiimba shairi maalum linalohusu CCM
 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiimba nyimbo za hamasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha juu moja ya kadi za Chadema zilizorudishwa  kisha wanachama hao kujiunga na CCM

No comments:

Post a Comment