Pages

Monday, June 23, 2014

URENO WATOA DROO YA 2 KWA 2 NA MAREKANI,JE WATAFUZU 16 BORA?


Kitu cha mwisho: Mchezaji wa Ureno aliyetokea benchi, Varela akipiga kichwa na kuuzamisha mpira wavuni akiisawazishia nchi yake na kulazimisha sare ya 2-2 katika dakika ya 95.
ZIKIWA zimesalia sekunde 5 tu mpira kumalizika, mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaddo alifanya maajabu katika fainali za kombe la dunia.
Wakiongoza 2-1 Marekani wakiwa chini ya kocha Jurgen Klinsmann walicheza soka zuri na kukaribia kuwatupa nje ya michuano Ronaldo na Ureno yake ili waungane na England.
Lakini kiungo wa Marekani, Michael Bradley-ambaye alicheza soka la kuvutia-alishindwa kumiliki mpira katikati ya uwanja katika dakika ya 95 na kushuhudia Ronaldo akichukua gozi na kupanda nalo upande wa kulia na kupiga krosi murua iliyozamishwa kimiani na nyota aliyetokea benchi, Silvestre Varela na kumuacha mlinda mlango Tim Howard akiwa hana la kufanya.
Mioyo ya Wamarekani ilivunjika ghafla. Sasa wanajiandaa kwenda Recife kupambana na Ujerumani siku ya alhamisi, lakini wanajua kundi limekuwa wazi.
Ureno wanatakiwa kukaza watakapokutana na Ghana ili angalau waendelee kuishi nchini Brazil.


Hakuna kitu kingine zaidi ya nyavu: Kichwa cha Varela kilimuacha mbali kipa wa Marekani Tim Howard


Kazi bado: Goli la Varela limewafanya Ureno wawe na matumaini ya kufuzu hatua ya 16 nchini Brazil.


No comments:

Post a Comment