Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema mashambullio
yaliyotokea katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la
wapiganaji wa Al Shabaab bali ni watu wanaoihujumu Kenya.
Rais Kenyatta ameyasema hao muda mfupi uliopita wakati
akilihutubia taifa la Kenya baada ya mashambulio mawili yaliyotokea Mpeketoni
juzi na jana.
Rais amewataja pia wanasiasa na baadhi ya maofisa kuhusika
katika mashambulio hayo ambapo baadhi yao wameachishwa kazi tayari na
watachukuliwa hatua kali ikiwemo kushitakiwa.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kuhusika na shambulio la juzi
usiku ambapo watu takribani 50 waliuawa.
No comments:
Post a Comment