Mfanyakazi wa ndani, miaka 14 mkazi wa kijiji cha Mdenge, Kata ya Likombe katika Wilaya ya
Mtwara, amebakwa na mwajiri wake usiku wa kuamkia jana na kumsababishia maumivu
makali na kisha kutokomea kusikojulikana.Akiongea juzi Jumatatu Juni 16, 2014, Mama mzazi wa
mtoto huyo, mwenye umri wa miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu
hayo siku nne tangu aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina
moja la, Sharifu (42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha
Alosko mkoani humo.Amebainisha kuwa, mtoto wake alipata
kazi ya kufanya kazi za
ndani kwa mwajiri huyo Juni 12, 2014 ambapo ilipofikia usiku wa kuamkia leo
mtoto huyo aliamua kutoroka nyumbani kwa mwajiri wake anayeishi na mke wake
bila kuaga kutokana na hofu ya kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na
kukimbilia nyumbani kwao.
“Alivyopata kazi anasema hii sio mara ya kwanza kufanyiwa
hivyo hii ni mara ya pili, usiku wa kuamkia Jumamosi ya Juni 14, 2014
alimuingilia mtoto wangu na alipomwambia atatoa taarifa akamwambia asiseme kwa
mtu yeyote kwani atamfanya kama mtoto wake, sasa leo tena amemuingilia.
“Nimemkuta yule mama aliyekuwa anafanya kazi kwake amesema
alihisi kuwa kuna huo mchezo lakini aliogopa kuniambia tangu Jumamosi”
alisema mama wa
mtoto.
Kwa upande wa mtoto huyo, amesema
,“Nilikuwa nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa maana alisema nisipige kelele”
,“Nilikuwa nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa maana alisema nisipige kelele”
Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo
katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba
Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi
kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha
makubwa.
Mtandao ulimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Zelothe
Stephen, ambaye hakupatikana kupitia simu yake ya mkoni baada ya kuita bila
kupokelewa, huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa wakigoma kuongelea suala hilo
wakidai hawajui alipo ndugu yao licha ya kushangazwa na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment