Pages

Friday, June 20, 2014

Ridhiwani ateka! mamia wafurika kwenye mikutano yake Singida

DSC09545

Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa, Ridhiwani Kikwete akihutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Itigi jimbo la Manyoni magharibi.
ZIARA ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM (NEC) Taifa, Ridhiwani Kikwete, aliyoifanya katika jimbo la Manyoni magharibi mkoani Singida hivi karibuni, imefunika kwa kuhudhuriwa na mamia ya wana CCM na wanachi kwa ujumla, kitendo ambacho hakikutarajiwa.
Wananchi hao wameenda mbali zaidi, kwa kudai kwamba Ridhiwani ambaye ni mbunge wa jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani, uwezo wa hotuba zake utamwezesha kumudu vema kuvaa viatu vya baba yake katika medani ya  kisiasa.
DSC09505
Ujio huo wa Kikwete,umeweza kuwaingiza wanachama wapya  wa CCM 359.Kijiji cha Gurungu 161,Sanjaranda 118 na 80 Itigi mjini.
Katika nyakati tofauti, MNEC huyo amewakumbusha wanachama wa CCM, kulipa ada za uanachama kwa wakati  ili pamoja na kuimarisha uchumi wa chama, mhusika ajijengee mazingira mazuri ya kuchaguliwa na kuchagua.

 
Akifafanua, amesema uhai wa chama chochote pamoja na vya kisiasa, unategemea kwa kiasi kikubwa ada za wanachama wake.
“Mwanachama CCM usipolipa ada kwa wakati, kwanza unakosa sifa ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Pia unakosa sifa ya kupiga kura na mbaya zaidi, ni kwamba unadhoofisha nguvu na uhai wa chama chako cha CCM .  Sidhani kama yupo mwanaccm ambaye anaweza kukosa ada ya mwezi ya shilingi moja tu”,alifafanua.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo,Kikwete  amesema demokrasia ya kweli na pana ipo ndani ya CCM na haipatikani kwenye chama cho chote cha siasa hapa nchini.
DSC09499
Mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Gurungu jimboni humo.
“Wote ninyi ni mashuhuda, kwenye vyama vya siasa rafiki, watu wanapeana nafasi za uongozi kiukooo, hakuna chaguzi huko chaguzi za haki na zenye uhuru mpana, zipo CCM pekee” amesema na kushangiliwa.
Mjumbe huyo amesema ili CCM iendelee kuwa na nguvu na kutesa katika chaguzi zote ni wanachama kulipa ada kwa wakati na kuhamasisha wananchi wengi kujiunga na chama hicho chenye sera zinazotekelezaka.
Katika hatua nyingine, Ridhiwani amewahimiza wananchi wa mkoa wa Singida, kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kupata katiba mpya itkayokidhi mahitaji ya wanachi kwa miaka 50 ijayo.
Amewataka wawe makini na siasa za sasa ambazo zingine zinahamamisha uwepo wa serikali tatu wakati kuendesha serikali mbili, ni tatizo kubwa.
DSC09543
DSC09553

No comments:

Post a Comment