Pages

Friday, June 20, 2014

MHE. MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA CHINA, CUBA, JAPAN, MSUMBIJI NA KAIMU BALOZI WA UJERUMANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing alipofika kwa ajili ya mazungumzo ambayo yalihusu pia ziara ya Makamu wa Rais wa China atakayoifanya hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 26 Juni, 2014.
Mhe. Balozi Lu akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao.
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi LU (hawapo pichani)

Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Cuba
Mhe. Waziri akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushrikiano kati ya Tanzania na Cuba. Tanzania na Cuba zinashirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na siasa.
Mhe. Membe akimsikiliza kwa makini Balozi Tormo.

 
Mazungumzo yakiendelea huku Afisa Mambo ya Nje, Bw. Lucas Mayenga akinukuu.

Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Japan
Mhe. Membe akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaki Okada alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Mhe. Balozi Okada akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Membe.
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nathaniel Kaaya akifuatili mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Okada (hawapo pichani)

Mkutano wa Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani
Mhe. Membe akimkaribisha ofisini kwake Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Bw. Hans Koeppel alipofika kwa mazungumzo na Mhe. Waziri kuhusu salamu za shukrani kwa Serikali ya Tanzania kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Frank-Walter Steinmeir kufuatia ziara yake ya mafanikio aliyoifanya hapa nchini mwezi Machi 2014
Mhe. Membe akipokea barua ya salamu hizo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini (hawapo pichani)


Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Msumbiji
Mhe. Membe akizungumza na Balozi wa Msumbiji hapa nchini, Mhe. Vicente M. Veloso alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Veloso na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe alipozungumza nao.

No comments:

Post a Comment