Hisia kali: Kiungo wa Ivory Coast , Serey Die akilia wakati wimbo wa Taifa lake ukiimbwa.
MCHEZAJI wa kamataifa wa Ivory Coast , Serey Die ameonesha uzalendo kwa nchi yake baada ya kucheza mechi ya kombe la dunia dhidi ya Colombia licha ya kufiwa na baba saa mbili kabla ya mchezo kuanza.
Kiungo huyo alimwaga machozi wakati wimbo wa taifa wa nchi yake ukiimbwa katika mchezo wa kundi C.
Wengi walijua pengine analia tu kwa kulipenda taifa lake, lakini kulingana na ripoti zinaeleza kuwa baba wa nyota huyo mwenye miaka 29 alifariki dunia muda mfupi kabla ya mechi kuanza mjini Brasilia.
Huzuni: Serge Aurier, Cheick Tiote na Didier Zokora wote walijumuika na kiungo huyo wakati wa huzuni kabla ya mchezo kuanza
Siku ya huzuni: Shujaa Die aliichezea Ivory Coast saa chache baada ya baba yeka kufariki dunia
Die alijaribu kuimba wimbo wa taifa lake, lakini kutokana na hisia kali alizokuwa nazo alishindwa kuzua machozi yaliyokuwa yanambubujika.
Beki Serge Aurier na mchezaji wa zamani wa Tottenham, Didier Zokora haraka walienda kumfariji mwenzao kabla ya mechi kuanza.
Nyota wa Newcastle, Cheick Tiote pia alienda kumpa mkono wa pole Die, ambaye kwa bahati mbaya mechi yenyewe ameshuhudia nchi yake ikifungwa mabao 2-1.
James Rodriguez na Juan Fernando Quintero waliifungia Colombia wakati mchezaji wa zamani wa Asernal, Gervinho alifunga bao la kufutia machozi kwa Tembo.
Die mwenye machungu ya kufiwa na baba yake alicheza mechi dhidi ya Colombia.
Die akichuana na mchezaji wa Colombia Juan Cuadrado mapema kipindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment