Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 26, 2014

Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa:Maelekezo kwa Walimu Ajira Mpya Kuchukua Nafasi za Ambao Hawakuwa na Sifa au Hawakuripoti Alikopangiwa

Utangulizi:
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI imewapangia vituo vya kazi ya ualimu walimu waliohitimu Vyuo vya Ualimu Mwaka 2013 kuchukua nafasi za walimu ambao hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa kwa ajira ya Machi 2014.
Baadhi ya waombaji hawakupangiwa vituo vya kazi kutokana na kutokuwa na sifa zinazostahili kuajiriwa katika utumishi wa umma kwa mfano:- umri na maombi kutoambatanishwa na vithibitisho muhimu n.k.
 
Maelekezo kwa Walimu Ajira Mpya
  1. Kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa kwa ajili ya kupangiwa vituo kuanzia tarehe 25/6/2014, hadi tarehe 30/6/2014.
  2. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 30/6/2014 hatapokelewa tena na nafasi yake atakuwa ameipoteza. 
  3. Walimu hawa ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi kufuatia Orodha iliyotangazwa Machi 2014 hivyo OWM – TAMISEMI haitafanya mabadiliko yeyote ya vituo katika orodha hii.


Imetolewa na: -
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA ZA MITAA NA SERIKALI


No comments:

Post a Comment