Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA, imewaonya wale wote
wanaotumia mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo
watakabiliwa na mkono wa sheria.Onyo hilo limetolewa jana mjini Arusha na Kaimu
Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, Dkt, Raynold Mtungahema,
alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha
chafu zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye mitandao.Nilipata kufafanua
yakua mtandao au kifaa chochote cha digitali kinapotumiwa visivyo kinaweza
kupelekea mtumiaji kujikuta akifanya uhalifu mtandao. Mifano katika hili
nilipata kueleza, pale mtumiaji anapotumia mtandao kutukana, kutishia na
kudhalilisha wengine mitandaoni anakua amefanya kinachoitwa
"Cyberbullying" ambacho ufafanuzi wa hili unaweza kusomeka
Kwa nchi za magharibi wamekuwa na kampeni mbali mbali zinazo
hamasisha kutokomeza aina hii ya uhalifu mtandao ambapo takwimu za ITU za mwaka
2013 zilionyesha takriban nusu ya wenye umri kati ya miaka 13 - 17 wamekua wana
athirikazaidi na "Cyberbullying".
Kwa Tanzania hapakua na tofauti, Mitandao imekua ikitumika
kusambaza taarifa za uongo, chuki na kudhalilisha wengine na hata baadhi
kutishia wengine kupitia mitandao (Simu pamoja na Komputa) kitu ambacho ni
hatari sana kwa usalama wa taifa lolote. Hili lilipelekea TCRA kuja na kampeni
ya "Futa delete kabisa" inayo hamasisha kutosambaza jumbe za chuki,
matusi au uongo ili kulinda amani ya Tanzania.
Aidha, hapo jana Katika muendelezo kuhakiki yakua kunakua na
matumizi salama ya mitandao Dr. Mtungahema amesema, matumizi ya mitandao ambayo
sio sahihi ni kosa la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara
moja na akawataka wanaochafuliwa kupitia
mitandao wafungue majalada polisi na mamlaka hiyo itasaidia kuwafuatilia
wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria .
Alisema mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika
kuchafua anaishi uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya
matumizi yasiyo sahihi ambayo
hayaruhusiwi.
Mtungahema,
amesema atakaebainika anatumia
mtandao kumchafua mtu mwingine huyo amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe
mbele ya vyombo vya sheria kwa kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa
mtuhumiwa atakaepatikana na hatia.
Aliongeza kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari
wahusika wameshatiwa mbaroni na
ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu mamlaka hiyo itaarifiwe.
Nchi wanachama wa jumuia
afrika mashariki zimeaanza kikao cha siku nne mjini Arusaha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi
wa chang moto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO,
Dakta Fracis Wangusi, amesema sekta ya
mawasiliano inakabilwa na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji
wa huduma za mawasiliano kwa haraka.
Wangusi ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya
mawasiliano nchini Kenya,amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka
mtandao wa analojia kwenda digital na
matumizi ya visumbusi kwa ajili ya luninga.
Aliongeza kuwa , sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya
kuwepo gharama kubwa za matumizi ya simu, usambazaji barua na vifurushi
kunakofanywa namashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao
haujapangiliwa ,matumizi ya vikwazo vya
kuchelewesha huduma ya haraka ya internet .
Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa
vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.
No comments:
Post a Comment