Wachezaji wa Ufaransa wakipongezana baada ya kufuzu hatua ya 16
TIMU ya Taifa ya Ufaransa imeitandika Uswisi mabao 5-2 usiku huu na kufuzu hatua ya 16 ya michauno ya kombe la dunia kutoka kundi E.
Karim Benzema amefunga goli kali dakika ya mwisho, lakini kwa bahati mbaya mwamuzi alikuwa ameshapuliza kipyenga kumaliza mchezo huo.
Mabao ya Ufaransa yamefungwa na Giroud dakika ya 17, Matuidi 18, Valbuena 40, Benzema 67, Sissoko 72.
Mabao ya Uswisi yamefungwa na Dzemaili katika dakika ya 81 na Xhaka dakika ya 87.
Katika mchezo wa kwanza wa kundi E, Uswisi walishinda mabao 2-1 dhidi ya Ecuador, wakati Ufaransa waliitandika Honduras mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment