Kitu cha mwisho: Mchezaji wa Ureno aliyetokea benchi, Varela
akipiga kichwa na kuuzamisha mpira wavuni akiisawazishia nchi yake na
kulazimisha sare ya 2-2 katika dakika ya 95.
ZIKIWA zimesalia sekunde 5 tu mpira kumalizika, mwanasoka
bora wa dunia, Cristiano Ronaddo alifanya maajabu katika fainali za kombe la
dunia.
Wakiongoza 2-1 Marekani wakiwa chini ya kocha Jurgen
Klinsmann walicheza soka zuri na kukaribia kuwatupa nje ya michuano Ronaldo na
Ureno yake ili waungane na England.
Lakini kiungo wa Marekani, Michael Bradley-ambaye alicheza
soka la kuvutia-alishindwa kumiliki mpira katikati ya uwanja katika dakika ya
95 na kushuhudia Ronaldo akichukua gozi na kupanda nalo upande wa kulia na
kupiga krosi murua iliyozamishwa kimiani na nyota aliyetokea benchi, Silvestre
Varela na kumuacha mlinda mlango Tim Howard akiwa hana la kufanya.
Mioyo ya Wamarekani ilivunjika ghafla. Sasa wanajiandaa
kwenda Recife kupambana na Ujerumani siku ya alhamisi, lakini wanajua kundi
limekuwa wazi.
Ureno wanatakiwa kukaza watakapokutana na Ghana ili angalau
waendelee kuishi nchini Brazil.
Hakuna kitu kingine zaidi ya nyavu: Kichwa cha Varela
kilimuacha mbali kipa wa Marekani Tim Howard
Kazi bado: Goli la Varela limewafanya Ureno wawe na
matumaini ya kufuzu hatua ya 16 nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment