Wasanii watakaopanda jukwaani katika Kilimanjaro Music Tour
wamewasili mjini Kahama kwa ajili ya show. Wasanii hao ambao ni Shilole,
Christian Bella, Madee, Mwana FA, AY, Rich Mavoko, Jambo Squad na Weusi
wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya Jumamosi katika uwanja wa halmashauri ya
Kahama kwa kiingilio cha Sh 2500. Mara baada ya kuwasili Mwana FA, AY, Rich
Mavoko na Shilole walifanyiwa mahojiano na Kahama FM ambapo walielezea namna
walivyojipanga kwa ajili ya show.
Ay na Mwana FA wakitaniana ndani ya Kahama FM leo |
Shilole akiongea na mashabiki wake kupitia Kahama FM leo
Shilole na Ay wakipiga picha ya Pamoja ndani ya kahama FM
No comments:
Post a Comment