Jumla ya watoto 963 wamelawitiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja
uliopita nchini Tanzania, huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni ukatili unaofanywa
dhidi yao pamoja na ukosefu wa mfumo bora na unaoeleweka wa kuwalinda watoto
dhidi ya hatari na majanga.
Kaimu mkurugenzi
mkuu wa kituo cha sheria na haki za binadamu, mwanasheria Harold Sungusia
(kushoto).Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Bw. Harold Sungusia, amesema hayo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
kimataifa ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo amesema takwimu hizo ni wastani wa
watoto wawili walikuwa wakilawitiwa kila siku.
Kwa mujibu wa Sungusia, wengi wa watoto hao, wamefanyiwa
kitendo hicho cha kikatili na ndugu zao wa karibu, ambao wamepewa jukumu la
kuwatunza ambapo kuna haja ya serikali kuhakikisha kuwa inaandaa mfumo utakaotoa
ulinzi kwa watoto hasa kupitia sheria ya haki na ulinzi wa mtoto ya mwaka 2009.
EATV
No comments:
Post a Comment