Askari wa uhamiaji wamewakamata watu 14 katika maeneo ya
Msasani jijini Dar es Salaam kutoka nchini India na Nepal ambao ni wahanga wa
biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambapo watu hao wameingia nchini
kinyume na taratibu za uhamiaji.
Kati ya watuhumiwa 14 watuhumiwa 12 ni wasichana ambao
waliletwa nchini kwa lengo la kufanya maonyesho ya nyimbo za asili lakini
wakajikuta wakingizwa katika biashara zingine ikiwemo kucheza muziki katika
nyumba za burudani.Kwa upande mtu anayedaiwa kuwaleta wasichana hao amesema
amewaleta kwa lengo la kufanya maonyesho ya muziki huku akipinga kuwa wasichana
hao hawatumii kinyume na hivyo.Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
mikoroshini msasani amewataka wakazi wa eneo hilo kujiepusha na tabia ya kukaa
na wageni bila ya kutoa taarifa mamlaka husika.Akithibitisha tukio hilo mkaguzi
wa uhamiaji Bw Dotto Romana amesema wanawashikilia watu hao na watachukua hatua
kulingana na mahitaji ya sheria.
No comments:
Post a Comment