Falcao akiwa na kocha wake Jose Pekerman kwenye mmkutano na
waandishi wa habari
MASHABIKI wa Colombia wamepagawa na taarifa kwamba nyota wao Radamel Falcao atazikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu nchini Brazil.
Kocha wa timu ya Colombia, Jose Pekerman jana jumatatu alitangaza kikosi chake katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Buenos Aires, nchini Argentina.
Falcao alipata majeruhi kubwa ya goti akiwa katika majukumu ya kuitumikia klabu yake ya Monaco mwezi januari, na ameachwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambapo kocha wake amesema hatakuwa tayari.
Nyota
huyo wa zamani wa Atletico Madrid alisajiliwa kwa dau kubwa mno majira
ya kiangazi mwaka jana, lakini kutokana na majeruhi aliyopata alikosa
matumaini ya kulitumia taifa lake katika fainali za kombe la dunia mwaka
huu.
Pekerman alisema wiki iliyopita kuwa
atasubiri mpaka siku ya mwisho na dakika ya mwisho ili kufanya maamuzi
juu ya Falcao baada ya kuona anaimarika kidogo kidogo, huku akionana na
madaktari wake, na mwisho wa siku, hapo jana alifanya maamuzi kinyume na
maneno yake.
No comments:
Post a Comment