Gari la Waziri wa
ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka likiwa katika
kituo cha polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kugonga punda
Waziri wa ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka amenusurika kifo baada ya
gari alilokuwa akisafiria kutoka Bukoba kwenda Dodoma kugonga mnyama punda
katika kijiji cha Wendele Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Walioshuhudia tukio hilo walisema lilitokea jana majira ya
saa 11 jioni ambapo lenye namba za
usajili STK 5857mali ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi
lililokuwa likiendeshwa na dereva Linusi Eliasi (42) liligonga
mnyama punda
aliyekatiza ghafla barabarani.
Akizugumza na
Malunde1 blog mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya amethibitisha
kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa waziri Tibaijuka alipata mshtuko baada ya
ajali hiyo na ofisi ya mkuu wa wilaya Kahama ilimpatia usafiri mwingine kwa
ajili ya kuhudhuria vikao vya bunge kufuatia gari lake kuharibika.Hata hivyo
mkuu huyo wa wilaya ya Kahama Benson
Mpesya amesema waziri Tibaijuka hakuumia
katika ajali hiyo na leo ameendelea na
vikao vya bunge mkoani Dodoma.
Akielezea zaidi
kuhusu ajali hiyo kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya
amesema Waziri Tibaijuka alikuwa na
baadhi ya wanafamilia wake katika gari hilo wakitoka Bukoba kwenda Dodoma kwa
ajili ya kuwahi shughuli za Bunge zinazoendelea.
Kamanda Kihenya amesema
baada ya kufika katika eneo hilo alikatisha punda katikati ya barabara
na katika harakati za dereva kumkwepa ndipo gari hilo lilipomgonga na kisha
mnyama huyo kufa papo hapo.Kihenya alisema kuwa katika ajali hiyo hakuna mtu
aliyeumia ila kuna baadhi ya watu waliopata majeraha madogo madogo ikiwa ni
pamoja na waziri huyo aliyepata mshtuko kidogo lakini baadaye hali yake
iliendelea vizuri.Hata hivyo katika hali
ya mshangao wa watu waliomiminika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa
ajili ya kumjulia hali waziri na kumpa pole lakini Waziri huyo na msafara wake
walikuwa wakipatiwa matibabu na wauguzi katika Hoteli moja iliyopo pembeni mwa
hospitali ya Wilaya Kahama.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog -Shinyanga
No comments:
Post a Comment