Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki
ya NMB Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu
kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika
kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mahakama imeukataa utetezi wa washtakiwa hao kuwa wakati wa
mauaji hawakuwa nchini, akisema ushahidi wa vinasaba (DNA), umethibitisha
walikuwapo nyumbani kwa mshtakiwa Kanje.
Moshi. Raia wawili wa Kenya, Samweli Saitoti (Saimoo) na
Michael Kimani (Mike), wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na
hatia ya kumuua polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), PC Michael Milanzi
mwaka 2007.
Raia hao ambao walipambana na polisi jijini Arusha kwa saa
sita wakijihami kwa silaha za kivita yakiwamo mabomu ya kurusha kwa mkono na
bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), walifanya mauaji hayo yaliyoambatana na
uporaji wa Sh239 milioni mali ya Benki ya NMB, Julai 11, 2007.
Pia, Jaji Kakusulo Sambo wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi,
amemhukumu Mtanzania, Calist Kanje kwenda jela miaka mitano kwa kuwasaidia
wauaji hao wasikamatwe na polisi baada ya kufanya mauaji.
Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Sambo alisema upande wa
mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya, Stella Majaliwa na
Ignas Mwinuka, umethibitisha mashtaka hayo pasipo shaka.
Jaji Sambo alisema ushahidi wa mashahidi 18, umethibitisha
kuwa raia hao wa Kenya ndiyo walioshirikiana kwa pamoja, kumuua polisi huyo
ambaye taifa bado lilikuwa likihitaji utumishi wake.
“Kulikuwa na hoja ya utetezi kuwa hawakutambuliwa kikamilifu
lakini PC Naftali Ashery aliyekuwa lindo na marehemu aliwatambua vilivyo wauaji
hao tena kwa ukaribu,” alisema. Alisema Mahakama imeridhika kuwa maungamo
waliyoyatoa mbele ya walinzi wa amani ambao ni mahakimu waliyatoa kwa hiari
bila kushurutishwa.Mahakama imeukataa utetezi wa washtakiwa hao kuwa wakati wa
mauaji hawakuwa nchini, akisema ushahidi wa vinasaba (DNA), umethibitisha
walikuwapo nyumbani kwa mshtakiwa Kanje.Jaji alisema kwa kuwa washtakiwa hao
walikwenda kwa Kanje na yeye akawasaidia wasikamatwe na kuwatorosha, hilo ni
kosa la kusaidia wahalifu baada ya kufanya mauaji.
Jaji Sambo alisema Kanje ndiye aliyeficha gari aina ya
Toyota Land Cruiser mali ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR),
lililotumika katika ujambazi huo na kwamba ushahidi wa wafanyakazi wawili wa
mshtakiwa huyo, unathibitisha kuwa ndiye aliyetoa maelekezo kwa dereva wake ili
akalitelekeze gari hilo eneo la Uwanja wa Ndege wa KIA.
Mahakama hiyo imeamuru kiasi cha fedha, Dola 8,145 za
Marekani na Sh1,769,000 walizokutwa nazo raia hao wa Kenya, zikabidhiwe Benki
ya NMB, Mwanga ziliko
No comments:
Post a Comment