Akaunti ya Twitter ya jeshi la Kenya pamoja na ile ya
msemaji wa jeshi hilo imevamiwa na wanaharakati ambao wanaonekana kupinga
ufisadi.
"Nyote ambao mmeiba pesa za wakenya , tunawaandama,''
haya ndio maandishi yaliyokuwa yamewekwa kwenye mtandao huo.
Kikundi cha wavamizi wa mtandao Anonymous,ndio wamekiri
kuwajibika na uvamizi huo.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa
Meja Emmanuel Chirchir,
hutumia akaunti yake ya Twitter kutoa taarifa kuhusu kundi la Al Shabaab.
Wavamizi hao walikosoa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta
wakisema kuwa inajali tu masilahi ya watu wenye ushawishi na haifanyi kazi ya
kutosha kukabiliana na uwindaji haramu pamoja na dawa za kulevya.Mwaka jana
kikundi cha wavamizi wa mitandao wanaojiita Anonymous, walivamia mtandao wa
wizara ya ulinzi ya Zimbabwe, na pia kuvamia mtandao wa chama tawala cha Afrika
Kusini ANC.
No comments:
Post a Comment