Maafisa wa masuala ya anga nchini Algeria wanasema wamepoteza
mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, iliyokuwa
katika anga ya Sahara. Shirika la habari za Algeria limesema ndege hiyo
ilikuwa ikisafiri kwenda Algiers na kupotea kwenye rada takriban dakika
40 baada ya kupaa kutoka jijini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso.
Air Algerie imesema imeanza shughuli za dharura kuitafuta. Indadhaniwa
kuwa na abiria 110 na wafanyakazi sita. Njia ya ndege hiyo ni kupitia
nchini Mali ambapo kuna mzozo unaendelea upande wa kaskazini.
No comments:
Post a Comment