Pages

Monday, July 7, 2014

DI MARIA AUMIA KUKOSA NUSU FAINALI


MSHAMBULIAJI wa Argentina, Angel Di Maria anatarajiwa kukosa mechi zilizonaki za timu yake za Kombe la Dunia baada ya kuumia jana katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Ubelgiji mjini Brasilia.
Di Maria atakwenda kufanyiwa vipimo baada ya kuumia dakika ya 33 jana, huku vyombo vya Habari Amerika Kusini vikiripoti kwamba mchezaji huyo wa Real Madrid ndiyo ameaga Kombe la Dunia.
Argentina ilitinga Nusu Fainali yake ya kwanza ya Kombe kla Dunia tangu mwaja 1990, lakini Di Maria hakushangilia ushindi na wenzake baada ya kuumia na kutoka kipindi cha kwanza.


No comments:

Post a Comment