Pages

Saturday, July 5, 2014

HOT NEWS: SOMA USHAHIDI 'KIGOGO WA TRA ALISIMAMIA OTOROSHAJI WA TWIGA' SOMA HAPA KWA MAKINI

  • Shahidi aieleza mahakama wakati wa kutoa ushahidi wake katika kesi ya kutorosha nyara hazo
image.jpeg
Moshi. Afisa mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Miraji Msakamali alishiki kusimamia utoroshwaji wa Twiga wanne kwenda Doha nchini Qatar kwa niaba ya TRA.
Hayo yalielezwa  jana shahidi wa 26 ambaye ni Afisa Mfawidhi wa TRA Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Ngovore Ngovore wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo.
Afisa huyo alitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo kwa kuongozwa na jopo la mawakili wa Serikali wakiongozwa na Evetha Mushi.
Shahidi huyo alidai kati ya Novemba 29 na 30,2010, alipata taarifa kuna wanyamapori hai walikuwa wamesafirishwa Novemba siku tatu nyuma yake bila kufuata taratibu.

Afisa huyo alidai baada ya kupata taarifa hizo, aliiandikia Kampuni ya Equity Aviation iliyoshughulikia mizigo hiyo na nakala kuzipa taasisi nyingine zilizopaswa kuhusika.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni Zoo Sanitary iliyopo chini ya Wizara ya Uvuvi na mifugo,  Kilimanjaro Aiport Development Company (Kadco) na Idara ya Polisi uwanjani hapo.
Katika barua hiyo, Zoo Sanitary walijibu kuwa usafirishwaji wa wanyama hao haukufuata taratibu, lakini Kadco wao wakadai hawaoni tatizo kwa vile taasisi zote zinazohusika zilishirikishwa.
“Kadco walimtaja Miraji Msakamali kuwa alikuwepo usiku huo wakati wanyama hao wakisafirishwa, lakini nilishangaa ilikuwaje mtumishi akarudi tena kazini”alidai shahidi huyo.
Hata hivyo, shahidi huyo alidai alipokutana na Msakamali ambaye sasa ni marehemu na kumuuliza, alikanusha taarifa hizo na kueleza hakuingia uwanjani kufanya kazi kama mtumishi wa TRA.
Shahidi huyo alidai kuwa ingawa kwa utaratibu, TRA ilipaswa kuwa na kumbukumbu za wanyama wote wanaoingia au kusafirishwa kwenda nje, katika usafirishaji wa Twiga hawana nyaraka zozote.
Alidai kuwa Novemba 24,2010, mshitakiwa wa tatu, Martin Kimati alifika ofisini kwake akiwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kihindi na kudai huyo Mhindi anatarajia kusafirisha wanyama.
Shahidi huyo alidai Kimath ambaye walikuwa wanafanya kazi wote Zoo Sanitary ndiye aliyezungumza kwa niaba ya huyo Mhindi lakini hawakuwahi kurudi tena ofisini kwake.

No comments:

Post a Comment